Jumanne 29 Aprili 2025 - 20:39
Ikiwa leo hatutaupazia sauti Umoja wa Ulaya, basi tutakuwa tumekubali kushirikiana na Israel

Mmoja wa maafisa wa ngazi za juu katika Umoja wa Ulaya amesema: Kufanya biashara na Israel ni fedheha ya hali ya juu kabisa, umoja wa Ulaya hapaswi kufanya tendo hili ovu. Msiwauzie silaha Israel.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza,, "Mark Botenga", mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa umoja wa Ulaya amesema: Ninapowaona viongozi wa umoja wa Ulaya wakiyakubali matendo ya Israel, hasira na chuki hutawala katika nafsi yangu. Si mimi tu, bali hata watu wote wa Ulaya wanaopenda ubinadamu wako hivi. Sasa ni wakati wa kupaza sauti na kutangaza waziwazi ili watu wote waisikie sauti yetu inayo wakilisha madai haki na chuki yetu dhidi ya matendo yanayofanywa na utawala huu dhalimu wa kinyama.

Kwa mtazamo wangu, umoja wa Ulaya unahusika katika matendo na jinai za Israel, kwa sababu ya baadhi ya mafungamano na utawala huu. Bunge limeutaka waziwazi umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo ili kusaidia upitishwaji wa misaada ya kibinadamu kuelekea Ghaza, na kuondoa vizuizi katika ukanda wa Ghaza, lakini hatuoni matokeo yoyote.

Kuhusu Ghaza, niseme kwamba hali ya kibinadamu ni mbaya sana, na takriban kwa muda wa miezi miwili sasa hakuna msaada wowote uliopita mipakani.

Wazayuni si tu wanaua raia wasio na hatia kwa mabomu na makusudi, bali hata wanakataa kabisa mahjtaji yote ya kimsingi na maisha kwa watu hawa wanyonge, Botenga aliendelea kwa kusema: Hiii ni jinai, huu ni uhalifu wa kivita, hili ni kosa dhidi ya ubinadamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha